Kifo cha aliyekua mwimbaji nguli
General Defao ambaye alikua mtunzi mashuhuri wa nyimbo za rhumba, pia mchezaji mahiri wa dansi ya kikongo amefariki dunia na kuacha uzuni mkubwa kwa ulimwengu wa dansi. Raia katika jiji la uvira mkoani Kivu ya kusini wamesikitishwa na kifo cha mwanamuziki huyo, kilichotokea nchini Cameroun.